Je, Construction Documents ni nini.?
- Working Drawings
- Bill of Quantities
- Specifications
1. Working Drawing
Baada ya mradi wowote ule kuwa designed uwe ni mradi wa daraja, culvert, jengo, barabara, tenki la maji, mfumo wa maji safi, n.k lazima designer atoe michoro.
Michoro ndio kitu pekee kinachokuwezesha wewe kama site engineer/technician kutimiza lengo la designer.
Mchoro ndio kitu kinachokupa picha halisi wewe unatakiwa ufanye kitu cha aina gani, kiweje na kiwe na muonekano upi.
Working drawing ndio blueprint (map) ya kukuwezesha wewe kufika unakotaka kufika, kufanya ujenzi unaotaka kuufanya.
Hauwezi kusimamia mradi kiusahihi bila kuwa na mchoro, itakuwa ni kitu ch ajabu mno wewe kama msimamizi wa site na haujui umuhimu wa michoro..
Working drawing zinatakiwa ziwe zionyeshe detail kwa upande wa Plan, Section na Elevation.
Plan view inaonyesha muonekana uliokamilika kwa upande wa juu..
Elevation inaonyesha muonekana uliokamalika kwa upande wa kulia, kushoto, nyuma na mbele.
Section inaonyesha detail za ndani zote na vipimo vyake.
Kazi nyingine za working drawings ni ;-
- Kukusaidia kupata vibali vya ujenzi
- Kukusaidia kuaanda B.O.Q
- Kukusaidia kuandaa specification
- Kukusaidia kwenye tendering stage
2. Bill of Quantities (B.O.Q)
B.O.Q inakusaidia wakati wa kuomba mradi kujaza rate na bei utakazo tumia kufanya huo mradi.
B.O.Q ndio muongozo wako wakati wa utendaji na usimamiaji wa mradi inakupa mwanga na picha kujua kama kazi unayofanya wakati huu umeifanya kwa hasara au faida.
B.O.Q pia inakupa nafasi ya kuandaa working schedule na schedule of Materials.
B.O.Q ndio reference wakati wa malipo... It's very absurd kwa site engineer au technician kuniambia unasimamia mradi na hauna B.O.Q au huja isoma B.O.Q vizuri na kuilewa ni kitu cha ajabu you know..😬😬.
3. Specifications
Specifications ndio documents ya tatu muhimu unayohitaji wakati unasimamia mradi site engineer/ technician.
Specification inakupa muongozo wa materials unazohitaji kwenye mradi, kiwango na ubor wa kazi unahohitajika.
Usichangenye mambo hapo specification na B.O.Q ni vitu viwili tofauti.
Na hizi ndizo Construction Documents Muhimu kwa Site Engineer/Technician katika Kusimamia Miradi ya Ujenzi.
Kupata sample ya hizi construction documents zote bofya ==> HAPA