Sekta 9 za Kiuchumi Ambazo Kila Civil engineer/Technician Anatakiwa Awekeze...!!💰💰

Wavuvi wote wanajua kitu kimoja ukitaka kuvua lazima uende sehemu ambako samaki wapo, huwezi sema unaenda kuvua na ukapata unachokitaka (samaki) sehemu yoyote tu!

Ukienda kuvua hata kama ni uvuvi halamu, lazima uende sehemu ambako samaki wapo not otherwise..

Vi vivyo hivyo intention ya kila mwizi kupata hela nyingi ni kuiba benki, Unadhani ni kwanini benki na sio sehemu nyingine?

Ni kwa sababu benki ndiko hela ziliko 😁😁...!!

Construction & engineering industry recently imeongezeka kuwa na watu wengi, nikimaanisha civil engineers na technician wamekuwa wengi mno (job markert demand low than supply).

Tuko kwenye nyakati ambayo unatakiwa ufahamu na ujifunze zaidi kuwekeza na sekta za kuwekeza ili wakati uanaendelea kupambana na job market upate pakuanzia na kuendeelea napo, kwa sababu hata ukipata hiyo ajira mshahara huwa hautoshi utajikuta majukumu au matumizi yanakuwa kuliko mshahara wako this is for sure..!!

Swali linakuwa gumu hapa, sawa kama ntataka kuanza kuwekeza either nikiwa masomoni au kwenye ajira niwekeze kwenye sekta zipi..?💭💭

Tunarudi kwenye mifano yetu miwili pale juu, ukitaka kuvua samaki lazima uende mahali ambapo samaki wapo si ndio....😀😀, Ukitaka kuiba hela nyingi lazima uende wapi? Lazima uende kuiba mahali ambako pesa nyingi zipo (Benki)...

It's the same idea kwako wewe civil engineer au civil technician unavyotafuta sekta za kuwekeza kukuza kipato chako lazima uwekeze kwenye sekta ambazo zimethibitishwa kukurudishia wewe thamani yako ya uwekezaji na kukuzalishia pesa zaidi.!!

Hapa siongelei KUBET, FOREX, CRYPTOCURRENCY n.k naongelea sekta zinazozalisha ambazo zimethibitisha kutokutetereka miaka na miaka na kuzalisha matajiri wakutosha waliowekeza kwenye hizo sekta.

Asikudanganye mtu kwamba unaweza kufanya kila biashara au ukawekeza kwenye sekta yoyote na kupata mafanikio, kwenye makala hii utajifunza sekta kuu 9 za kiuchumi ambazo wewe kama civil engineer au civil technician unatakiwa uanze kuwekeza huko ili kupata matokeo na kupambana na janga la uchache wa ajira..

Kabla hujaendelea kusoma makala hii zaidi naomba usapoti channel yangu ya YouTube ==> HAPA hii inanitia moyo kuendelea kuandaa makala zenye kukupa mwanga kama hizi...🙏👍

1. Sekta ya Fedha 💰💰

Navyoongelea sekta ya fedha ni sekta inayochangia kwa asilimia 18.7 ya Uchumi wa taifa source (TanzaniaWeb.Live), navyoongelea sekta ya fedha na maanisha makampuni yote yanayojihusisha na mambo ya kufanya menejimenti ya fedha, Kukopesha na Menejimenti za Asset (Mali).

Yaani Benki zote, Makampuni ya fedha, Makampuni ya Bima(Bima zote zile Magarai, Afya n.k), Makapuni ya Udalali (Brokeage Firms).

Mtu yoyote ambae amejitoa kuwekeza kwenye kutoa huduma sekta ya kifedha hata siku moja huwezi ona analala njaa..

Kwaio kuanzia leo anaza kufikiria kuwekeza kwenye sekta hii kama huna mtaji mkubwa anaza na kuwa wakala tu anayetoa huduma za kifedha, mtaji ukiongezeka fungua kamapuni ya kukopesha, kampuni ya bima n.k!!

Makampuni yote ambayo unajua yako kwenye sekta hii huwezi kuta nimaskini hata siku moja chukulia mfano shirika la bima ya Taifa (NHIF) unazania kama kila mwezi linachukua sh. 60,000 kwa kila mtanzania kwa wafanyakazi 6000730, ni shingapi kwa mwaka {60,000 * 6000730 * 12} hizo ni hesabu za juu juu tu majibu baki nayo hahaha..

Njoo kwa Mabenki NMB, CRDB n.k uoni kama mabenki Tanzania yanaongezeka mengi na ujiulizi ni kwa nini? 😃😃..

Ukitaka hela lazima ukae sehemu ambako hela ziko.!!

Kwaio kuanzia leo anza kuitilia maanani hii sekta usichukulie poa anzia popote kama Wakala, Muwekezaji wa mifuko ya pamoja, Muwekezaji binafsi n.k

2. Sekta ya Afya 

Vingine vyote vinatafuta ila Afya, Uhai na Uzima ni mmoja tu ukipoteza huo maake ndio basi, asikwambie mtu watu wako tayari kulipia chochote kile kuhakikisha wanakuwa na afya njema na wanaishi maisha marefu.

Ukienda hospitalini na ugonjwa wako hata kama wakutajie bei gani lazima utapambana tu uilipe ili uwe na afya njema, hata wakisema dawa inauzwa shingapi lazima utapambana tu ipatikane ili uwe na afya njema.

Sekta ya huduma za afya hauwezi kulala njaa hata siku moja, kwa sababu magonjwa changamoto za afya zipo na hazikwepeke kwa sababu ya hali ya hewa ,mitindo ya maisha n.k

Fikiria hata kuanzia duka la dawa, kuuza bidhaa zinazowasaidia watu matatizo mbalimbali ya kiafya (ziko nyingi mno mno hapa) kama mtaji mdogo tafuta kampuni lenye kujieweza na uwe wakala wao unauza dawa na wanakupa commision, fungua mahabara ya vipimo binafsi, fungua kituo kidogo cha afya, jenga kituo cha kuwalea na kuwajali wazee n.k

3. Sekta ya Elimu 📚📚

Msingi wa chochote kile ni maarifa na ujuzi, nchi ili iendelee inahitaji watu wenye ujuzi na utaalamu sekta ya elimu ni sekta inayoishi miaka na miaka na haiwezi kufa kwa sababu watu wanaongezeka na kuzaliwa kila inapoitwa leo, na watu wanahangaika kupata elimu na maarifa.

Unaweza kuona namna ya kuanzia popote kuandika vitabu vinavyotoa elimu kwa watu, kuanzisha shule za awali kwa watoto (daycare), shule za kati (primary) ukitoa huduma nzuri ya elimu hauwezi kosa wateja.

Kitu kizuri kinajiuza chenyewe....👍👍

4. Sekta ya Chakula na Vinywaji 🍲🍻

Wote tunafahamu mtu haishi kwa maneno tu bali na mkate, miomgoni mwa mahitaji makuu na ya muhimu kwa mwanadamu ni chakula, maradhi na mavazi.

Sekta ya chakula inajumuisha vitu mbalimbali kama kulima mazao ya chakula, kuuza mazao ya chakula, kutengeneza na kusambaza biashara za chakula zitazofanyia watu wepesi kwenye ratiba zao.

Huwezi wekeza kwenye sekta hii na ukatoka au ukawa mikono mitupu my friend..💰💰

5. Sekta Ufugaji 🐮🐷🐔

Hii ndio sekta yangu pendwa mno kuliko zote, kulingana na takwimu asilimia zaidi ya 65% za ajira zinatokea katika sekta hii usichukulie poa.

Ni sekta ambayo huwezi kukutana na tabu za TRA hata siku moja, ni wewe na watu unaowahudumia.

Unaweza wekeza kwenye sekta hii katika nyanja tofauti tofauti ikiwa ni pamoja na kuuza chakula cha mifugo, kuuza mbegu (breed) za mifugo, kutoa huduma ya dawa na matibabu kwa mifugo, kuuza vifaa vinavyorahisisha ufugaji, au kuwa mfugaji.

Na hauhitaji mtaji mkubwa wala elimu kubwa hapa mimi niliingia katika sekta hii mwaka 2019, ni baada ya kujifunza kitu kutoka kwa babu yangu the late mzee mamboleo mbugi aliyeishi kwa miaka 124 na alipata mafanikio sana kwenye sekta hii alikuwa mfugaji mkubwa wa ng'ombe na mbuzi.

Ila mimi binafsi nimejikita kwenye kufuga nguruwe na kuku kwa sababu zangu nyingi binafsi na wewe kama utahitaji ushauri hapa usione shida kunitafuta tukawasilina, na nilianza kufuga nikiwa kama mwanafunzi nikiwa ngazi ya Bachelor degree in civil engineering.

6. Sekta ya Usafiri na Usafirishaji 🏍🚍

Boda boda hata siku moja hawezi kaa njaa, bajaji hata siku moja hapawezi kupita patupu vi vivyo hivyo kwa vyombo vingine vya usafiri.

Huduma ya usafiri na usafirishaji ni kitu tunachohitaji kila siku kwenye maisha yetu kwa sababu watu wako kwenye movement mbalimbali za kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Unahitaji kutoka nyumbani kwenda ofisini (kazini) lazima utahitaji usafiri, unhitaji kutoka kwenda hospitalini lazima utahitaji usafiri tu, unataka kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine hauwezi tumia ungo 😄😄 utahitaji usafiri tu..

Kwaio ni sekta ambayo hauwezi kulala patupu angalia kama ni interest yako unaweza kuamua kuanzia hapa.

7. Sekta ya Makazi na Ujenzi 🏡👷

Kulingana na takwimu za za National Bureau Statistic Tanzania (Tuko watanzania kama millioni 61+ na makazi ni kama millioni 14+) kwaio unaona kabisa uhitaji wa makazi ulivyokuwa mkubwa watu wanahitaji mahali salama pakuishi na kufanya makazi 

watu wanahitaji miundombinu mbalimbali ya maji, barabara, majengo ya hospitali, biashara n.k

Kwaio unaweza kuamua kuanzia popote tu kama dalali wakuwatufuti watu nyumba nzuri za biashara, kukodisha viwanja, kupangisha watu nyumba, kuwa na kampuni ambayo inajihusisha na mambo ya ujenzi n.k

8. Sekta ya Technology 

Nikisema technology siongelei mambo vitu kama google, amazon, facebook n.k dunia sasa inaendelea kwa kasi mno mbinu zinazotumika kwenye ujenzi sio kama za miaka ya nyuma watu wanatumia technology za kisasa zaidi kama kutumia material ambazo ni improved na easy to use.

Watu wanatumia mitambo ya kisasa katika shughuli zao za uzalisha kwaio wewe ukijikita katika kuwaletea watu technology mpya inayowapa mafaniko kwa haraka lazima watakuwa tayari tu kuilipia kwa gharama yoyote ile.

9. Sekta ya Entertainment na Recreation 

Burudani na Vivutio vya Kupumzika na Kuenjoy, Hivi unajua kama watu wanapenda starehe kuliko kazi 😁😁, kama ulikuwa ulijui ndio maana na kwambia huoni wasanii wengi wanatajirika ni kwa sababu wako watu waliona kama hii sekta inalipa na wakaamua kuwekeza huko.

Wewe unaweza ukawa unajiuliza sasa hapa mimi naanzia wapi anzia popte tu kama kuwa mshereheshaji, kuuza movie na series , kuwa na bar nzuri yenye kutoa huduma za kuvutia kwa watu, ni vitu fulani unavyoona ni vya kipuuzi ila i promise you hauwezi kukaa patupu.

Nasisitiza tena watu wanapenda starehe na mapumziko kuliko kazi....😄😄!!

Nashukuru kwa kusoma makala hii mpaka mwisho kama unaswali lolote post kwenye comment section kuendelea kujifunza zaidi kama, kuna kitu cha kuongezea unatamani na wengine wajue post kwenye comment section.

Hizi ndio sekta kuu 9 unazoweza kuwekeza wewe kama civil engineer au civil technician na zikakupa mafaniko wakati wote.. share na marafiki kama umejifunza kitu!!

Soma makala nyingine hizi kujifunza zaidi.. 

Previous Post Next Post

Contact Form