Hatua kwa Hatua: Jinsi ya kufanya makadirio sahihi ya cement, mchanga, kokoto na maji kwa zege gredi 20 (M20) ukiwa site.

Kuwa na uwezo wa kufanya makadirio ya materials za ujenzi site ni ujuzi ambao kila msimamizi wa site anatakiwa kuwa nao 👌👌 hata kama sio kwa undani sana ila ni muhimu ni ujuzi namba tano, kati ya aina kuu 5 za ujuzi muhimu ambao msimamizi wa site anatakiwa kuwa nao site civil engineer/technician...💪💪

Kabla ujaendelea kusoma makala hii naomba muda wako kidogo sapoti chaneli yangu ya YouTube bofya ==> HAPA hii inanipa moyo na faraja mimi kukuandalia makala za kujifunza kama hizi.

Pia unaweza kupitia makala hizi kujifunza zaidi;

    Tunaendelea. . . . 

    Lengo la makala hii ni kukupa muongozo wewe kama fundi, site technician/engineer au msomaji jinsi ya kufanya makadirio ya cement, mchanga kokoto  na maji kwenye zege gredi 20 (M20)..

    Vitu utavyojifunza kwenye makala hii..

    • Je, zege gredi 20 (M20 au C20) ni nini.?
    • Je, kuna umuhimu gani unapo zingatie ratio sahihi za zege site?
    • Je, zege gredi 20 (M20) inatumika wapi?
    • Materials zinazohitajika kwenye zege gredi 20 (M20) na viwango vyake
    • Je, tunakadiria vipi cement, mchanga , kokoto na maji kwenye zege gredi 20 (M20)?

    Je zege gredi 20 (M20 au C20) ni nini.?

    Zege gredi 20 (M20) ni nominal mix (Kwa maana ya kwamba ni ratio ambayo inafahamika hivyo na ipo hivyo hata usipofanya concrete mix design) utapata majibu kama ukitumia materials yenye viwango sahihi yaani cement, mchanga na kokoto.

    Tukisema M20 tunamaanisha vitu viwili (M =>ikiashiria Mix, C=> ikiashiria Class & 20 => ikiashiria compressive strength ya zege baada ya siku 28, ikipimwa kwa N/mm²)

    Zege gredi 20 (M20) ina kuwa na mchanganyiko wa 1: 2: 4 tukimaanisha cement (1), mchanga (2) & kokoto (4)
    Kwa kutumia ndoo kubwa  mfuko 1 wa cement, mchanga ndoo kubwa 3 na kokoto ndoo  kubwa 6
    Kwa kutumia ndoo ndogo mfuko 1 wa cement, mchanga ndoo ndogo 6 na kokoto ndoo ndogo 12
    Na kiwango cha maji ni (Maximum water cement ratio kwa uzito ni 0.60)

    Je, kuna umuhimu gani unapo zingatie ratio sahihi za zege?

    Umuhimu wa kufuata uwiano sahihi wa viungo vya zege ni kwamba inakuwezesha kupata kiwango kinachohitajika cha compressive strength bila kukumbana na changamoto yoyote. 

    Hii inahakikisha uimara na ufanisi wa miundo yako, hivyo kutoa matokeo bora na kudumu kwa muda mrefu.

    Je, zege gredi 20 (M20) inatumika wapi?

    Zege gredi 20 (M20) inatumika kwenye structural application works, ni kimaanisha linatumika kwenye ujenzi wa nguzo(column), beam (bimu) na structures nyingine zote zinazobeba mzigo mzito unaobebwa na muunganiko wa uwezo kutoka kwenye zege (concrete) na nondo (reinforcement).

    Kwa jina moja tunasema reinforced concrete work (zege lenye nondo).

    Materials zinazohitajika kwenye zege gredi 20 (M20) na viwango vyake

    Cement: Tumia Ordinary Portland Cement (OPC), au High Alumina Cement au Rapid Hardening Cement

    Mchanga: Hakikisha mchanga ni msafi.

    Kokoto: Tumia kokoto zenye ukubwa wa juu zaidi wa 3/4" (20mm) au chini ya hapo. Zinapaswa kuwa na uwezo wa kujitosheleza, safi, na zisizo na vumbi, vifaa laini, udongo, au vitu vingine vya kigeni. Hakikisha zinatoka kwenye chanzo kinachojulikana na kilichopimwa.

    Je, tunakadiria vipi cement, mchanga , kokoto na maji kwenye zege gredi 20 (M20)?

    Hatua ya kwanza ni kutafuta volume (wet volume) ya zege hiyo gredi 20 (M20) ya mahali unapotaka kuli cast ilo zege,

    Unaweza kutizama video hio hapa chini kuona mfano jinsi ya kutafuta wet volume kwenye column..

    Hatua ya kwanza kupata : Kiwango sahihi cha zege linalohitajika

    Dry volume = Wet volume x 1.54 (1.54 ni ongezeko la zege kutokana na factors kama wastage, shrinkage, compaction factors etc.)

    Hatua ya pili kupata: Kiwango sahihi cha cement inayohitaji

    Cement quantity in volume = Dry volume x Ratio of cement/Sum of mix ratio
    Idadi ya mifuko ya cement = cement quantity in volume x 1440/ 50

    Hatua ya tatu kupata: Kiwango sahihih cha mchanga kinachohitajika

    Sand quantity in volume = Dry volume x Ratio of sand/Sum of mix ratio

    Tripu za mchanga zinazohitajika = Sand quantity in volume/ Tipper capacity ( kama tipa ina chuka ujazo wa cubic mita 3, 4, 4.5, 15 etc)

    Hatua ya nne kupata: Kiwango sahihi cha kokoto kinachohitajika

    Aggregate quantity in volume = Dry volume x Ratio of aggregate/Sum of mix ratio

    Tripu za kokoto zinazohitajika = Aggregate quantity in volume/ Tipper capacity (kama tipa ina chuka ujazo wa cubic mita 3, 4, 4.5, 15 etc)

    Hatua ya tano kupata: Kiwango cha maji kwa ujazo kinachohitajika

    Kiwango cha maji = Water cement ratio x Cement quantity in volume

    Tizama video hii hapa chini kuona mfano mpaka mwisho (Step-by-step calculation example for 1 meter cubic of concrete)

    Kwa zege ambalo siyo nominal mix kama vile M30, M35, na kadhalika, unahitajika kufanya 'concrete mix design.' Hatua hii ni muhimu ili kuhakikisha uwiano sahihi wa zege na kupata compressive strength inayohitajika kulingana na mazingira na materials unazotumia hapo sehemu. 

    Tazama video hii hapa chini kujifunza kwa undani jinsi ya kufanya 'concrete mix design' kwa usahihi na ufanisi, na kuhakikisha uimara na ubora wa zege lako.

    Kupata concrete design excelsheet bofya ==> HAPA

    Kupata reference books & manual za concrete bofy ==> HAPA

    Kama umenufaika na makala hii, tafadhali shiriki ili iweze kuwafikia wengine zaidi na kuwasaidia kama ilivyokusaidia wewe. Pia, tungependa kusikia mawazo yako! 

    Acha maoni yako au uliza swali katika sehemu ya maoni. Ushirikiano wako unathaminiwa na tunatarajia kujadili zaidi na wewe.

    Happy learning...✌✌

    Previous Post Next Post

    Contact Form