Jinsi ya Kukadiria Mchanga na Cement Unavyohitaji kwa Ajili ya Kufyatulia Tofari za Block

Je, tuna aina ngapi za matofari Tanzania?

Tizama video hii iliyotolewa na shirika la viwango tanzania TBS kujua aina kuu za tofari yanayofaa katika ujenzi tanzania.


Kwa tanzania, ujenzi  wa nyumba mijini iwe ni ghorofa (multi-storey building), matenki ya maji, au nyumba za kawaida kwa kiasi kikubwa tunatumia matofari ambayo ni solid block nchi (6").

Solid block nikimaanisha matofari ambayo hayana huwazi (void) yoyote na yanatengenezwa kwa mchanganyiko wa cement na mchanga au cement na crusher dust au cement, chippings na mchanga.

Solid block ni tofari ambayo vipimo vyake ni (450mm urefu x 230mm upana x 150mm unene) yaani nchi (18") kwa nchi (9") kwa nchi (6").

Kama mkandarasi ukiwa umepata kazi ya ujenzi au wewe mwenyewe ukiwa unatamani kufanya ujenzi wako lazima utalazimika either kununua hizo tofari au kufyatua mwenyewe ili kukamilisha kazi yako.

Kipi bora kati ya kununua tofari na kufyatua mwenyewe.?

Faida ya tofari za block za kununua:

i. Zinafanya kazi yako ikimbie na kufanyika kwa kasi kwa sababu material yanakuwepo on time.
ii. Zina save muda wako na changamoto zinazotokana na ufyatuaji wa tofari

Hasara ya tofari za block za kununua:

i. Bei huwa ni kubwa
ii. Kutokuwa na kiwango cha ubora unachohitaji

Kama mazingira yana ruhusu basi unaweza kuchukua za kununua ila tu uhakikishe unazipima ubora wake, ila kama unaona mazingira haya ruhusu unapotaka kufanya ujenzi yaani bei ya tofari ni kubwa, lakini pia hata kiwango cha hizo tofari ni mdogo na muda una kuruhusu basi ni vizuri kufyatua tofari zako mwenyewe ili kujihakikishia ubora na kiwango kinachotakiwa kwa ajili ya kazi yako.

Kama utaamua kufyatua tofari zako mwenyewe na unapata changamoto jinsi ya kufanya makadirio ya cement na mchanga unahohitajika ili kufanikisha zoezi lako la kufyatua tofari kwa ajili ya kazi yako basi hii makala ipo kwa ajili yako..👉✌

Soma mpaka mwisho kujifunza hatua kwa hatua jinsi ya kufanya makadirio ya mchanga na cement unavyohitaji kwa ajili ya kufyatua matofari yako.

Kabla ujaendelea kusoma makala hii naomba muda wako kidogo sapoti chaneli yangu ya YouTube bofya ==> HAPA hii inanipa moyo na faraja mimi kukuandalia makala za kujifunza kama hizi.

Pia unaweza kupitia makala hizi kujifunza zaidi;

Jinsi ya Kukadiria Mchanga na Cement Unavyohitaji kwa Ajili ya Kufyatulia Tofari za Block

Hatua ya kwanza: Vitu vya msingi unavyotakiwa kuvifahamu kwa ajiri ya makadirio ya idadi za tofari 

Je, ni matofari mangapi unahitaji kwa ajili ya ujenzi wako. (Chukulia mfano tunahitaji matofari: 3000)

Kwa mfuko mmoja wa cement unatakiwa utoe tofari 25 (Ni kiwango kinachoshauriwa kabisa kwa mchanganyiko wa uwiano 1:6 mpaka 1:10)

Hatua ya pili: Tafuta idadi ya mifuko ya cement inayohitajika.

Mfuko 1 tunapata tofari 25, kwa tofari 3000 ni mifuko 120

Hatua ya tatu: Tafuta  kiasi cha mchanga kinachotakiwa kwa ajili ya kufyatua matofari.

Volume tofari moja = urefu wa tofari x upana wa tofari x unene wa tofari = 0.45 x 0.23 x 0.15 = 0.015525m3

==> Volume jumla ya matofari yote = 3000 x 0.015525 = 46.575m3 ------- (i)

Volume jumla ya mifuko yote ya cement, mfuko mmoja wa cement volume yake ni 0.03472m

==> Volume jumla ya mifuko yote ya cement = 120 x 0.03472 = 4.167m3 -------(ii)

Volume ya cement + Volume ya mchanga = Volume ya matofari yote yaliyokamilika

==> Volume ya mchanga = 46.575m3 - 4.167m3 = 42.408m3 

Chukulia mfano tungepata gari tipa lenye uwezo tani 5 lenye capacity ya kuchukua 3.8m3
Kwaio tungeagiza tripu = 42.408m3/ 3.8m3 = 11.16 ~ 11

Cha kuzingatia zaidi ni kupata gari lenye viwango na uwezo unaotaka wewe mfano niliotumumia mimi ilo tipa la 3.8mnimetoa mfano tu, kingine zingatia ongezeko la mchanga ukiwa mbichi na mkavu (bulking of sand).

Hitimisho kwa matofari 3000, tungehitaji :

==> Mifuko 120  ya cement
==> Tripu 11 za mchanga kwa gari lenye kubeba 3.8m3

Je, wajua kama unaweza pata tofari kutokana na taka za plastiki tunazozalisha nyumbani.? 🙈

Angalia video hii kujifunza jinsi ya kutengeneza matofari yanayotokana na taka za plastiki. 

Video inaeleza hatua kwa hatua mchakato wa kubadilisha taka za plastiki kuwa matofari yenye nguvu na yanayodumu. 

Utajifunza jinsi plastiki hutayarishwa, kuchanganywa na vifaa vingine, na hatimaye kufinyangwa kuwa matofari. 

Mbinu hii ni muhimu katika kusaidia kupunguza uchafuzi wa mazingira na kutoa suluhisho la ujenzi ambalo ni rafiki kwa mazingira.




Nashukuru kwa muda wako kusoma mpaka kufikia hapa mwisho...🙏
Kupata civil engineering excel-sheets bofya ==> HAPA
Kupata reference books & manual za tofari bofya ==> HAPA
Kupata site documents mbalimbali bofya ==> HAPA
Kama umenufaika na makala hii, tafadhali shirikisha ili iweze kuwafikia wengine zaidi na kuwasaidia kama ilivyokusaidia wewe. Pia, tungependa kusikia mawazo yako! 

Acha maoni yako au uliza swali katika sehemu ya maoni. Ushirikiano wako unathaminiwa na tunatarajia kujadili zaidi na wewe.

Happy learning...✌✌

Jifunze ==> Hatua kwa hatua: Jinsi ya kufanya makadirio sahihi ya cement, mchanga, kokoto na maji katika zege gredi tofauti tofauti.


Previous Post Next Post

Contact Form