Aina kuu 5 za ujuzi muhimu unaotakiwa kuwa nao civil site engineer/technician ili kusimamia na kumeneji kazi site.

Asilimia zaidi ya 85% ya vitu tunavyosoma tukiwa chuoni ni theory na sehemu ndogo tu ndio practical.

Kiasi mtu anapomaliza masomo anakuwa hafahamu ujuzi  gani hasa.?? 👀 utamsaidia kupambana na kazi za site.


Kabla ujaendelea kusoma makala hii naomba muda wako kidogo sapoti chaneli yangu ya YouTube bofya ==> HAPA hii inanipa moyo na faraja mimi kukuandalia makala za kujifunza kama hizi.


Kabla ya kupata ajira permanent ya serikali nilipata bahati ya kufanya kazi na wakandarasi zaidi ya watatu kwa vipindi tofauti tofauti ambao ni:
  • Videfca Construction & Technical Services Ltd 
  • Maclesence Investment Company  Limited 
  • Mtwivila Traders & Construction Company Ltd  
  • Hano Construction Company Limited n.k
Kwa kipindi hicho nilikutana na changamoto nyingi mno.. 😕😕 zikiwemo zifuatazo..

Siku ya kwanza nimefika tu nikapelekwa site hafu hata nnachotakiwa kukifanya site nilikuwa sijui ni nini..😆🙈 najua utakuwa unapata picha kama hiyo na maanisha nini hapo..💭💭 mafundi wanategemea maelezo kutoka kwako hafu na wewe hujui chochote

Kuna site nyingine nilijikuta mimi ndio msimamizi na meneja wa kila kitu lakini hata pakuanzia nilikuwa sijui ni wapi.?😫😫

Hii yote ni kutokana nilikuwa sifahamu aina za ujuzi ambao ungekuwa ni msaada kwangu kusimamia site ila baada ya muda nilikuja kufahamu skills nilizokuwa nahitaji  ili kusimamia site kwa mafanikio.

Kwa utafiti uliofanya na watu fulani hizi ndizo aina kuu 5 za ujuzi unaohitaji wewe kama civil site engineer/technician na asilimia za uhitaji wake ili uwe tayari kusimamia kazi site.

Aina kuu 5 za ujuzi muhimu unaotakiwa kuwa nao civil site engineer/technician ili kusimamia na kumeneji kazi site.

                 [Image credit: digiqc - (source: https://www.digiqc.com)]

1. Kusoma michoro ya kazi site (Working drawing Interpretation) - (90.4%)

Kama inavyofahamika lugha ya wahandisi ni mchoro..😊

Huwezi kufanya kazi yoyote ile kama hujaelewa mchoro, kusoma mchoro ni zaidi ya asilimia 40% ya kufanyika kwa kazi.

Majibu ya mchoro ndio yanatoa muongozo wa vitu vingine vyote kufanyika kama setting out, excavation n.k

Kama hujui kusoma mchoro huwezi kujua kama ulichofanya ndio kinachotakiwa au siyo.

Na hamna mradi au kazi ya civil engineering inayofanyika bila mchoro (working drawing), mchoro ndio base line yakukuongoza wewe na hata client/consultancy atakupima kulingana na mchoro ulivyo na unavyolipwa utalipwa kulingana na vipimo vya mchoro. 

Unachotakiwa kama ni msimamizi wa barabara tafuta michoro mingi kadri uwezavyo na ujifunze kuisoma, kama ni majengo pia vivyo hivyo n.k..

2. Kufatilia na kujua ubora wa kazi na material site (Quality check and control) - (72.1%)

Ili ufanye kazi ya site kwa ubora lazima ujue kuzingatia ubora wa material zinazotumika na kazi unayoifanya.

Na kitu kinachokupa muongozo hapa ni specifications na standard code zinazohitajika kwa ajili ya kazi.


Kwaio kama ni unasimamia kazi ya barabara lazima ujue vizuri specifications zote za material yanayohitaji na kazi inayohitajika kisha uzingatie hivyo katika utendaji.

Cha muhimu hapa ni kusoma specifications na standard code uzijue in and out..💪

3.Setting out, surveying & levelling - (58.7%)

Hakuna structure inayojengwa hewani 😀😀

Baada ya kuweza kusoma mchoro lazima ujue kile kilichopo kwenye mchoro unakiamisha vipi kikae ardhini..😄

Hapa ndiopo umuhimu wa kujua setting out, line out, staking, surveying na levelling unapokuja

Vibarua kazi yao ni kufata maelekezo yako kwamba ichi kina kaa hivi ichi hivi n.k

Lazima ulijue ili, ili kuweza kusimamia kazi yako site.

4. Kufanya makadirio ya kazi na gharama (Quantity estimations) - (49%)

Ili ujenzi na kazi ya site iendelee utahitajika kufanya ordering ya material kwaio lazima ujue kuandaa schedule of material, kufanya makadirio ya viwango vya materials vinavyohitajika na gharama zake ili uiingiliwe wala kufanya kazi kwa hasara.


Ujuzi huu unasaidia pia hata katika work valuation, lazima ujue kupima na kufanya measurements za kazi yako site uweze kulipa vibarua, mafundi lakini pia hata wewe kulipwa


5. Usalama mahali pa kazi (Safety matters) - (40.4%)

Asilimia takribani 15% za ajali zinazotokea duniani zinatokana na ujenzi kwaio lazima ulifahamu ilo na kulisimamia kwa sababu OSHA wanapiga faini usipokuwa makini kwaio wewe kama msimamizi wa site ilo ni muhimu kulijua.

Kwaio ujuzi kuhusu usalama wa kazi ni kitu muhimu mno mno.

Kwaio unatakiwa kumkumbusha kuvaa vifaa kinga kama reflectors, safety boots, elements  ili kuepukana na ajari za site.

Simamia profesional yako inavyotakiwa💪💪usionekane mbabaishaji, site engineer/technician...!!

Hitimisho hizo ndio aina kuu tano (5) za ujuzi muhimu unaotakiwa kuwa nao civil site engineer/technician ili kusimamia na kumeneji kazi site.

Kama umenufaika na makala hii usisahau kuweka comment  yako & share ili iwasaidie na wengine... 🙏🙏


Pia naomba muda wako mchache kusapoti channel yangu ya youtube bofya ==> HAPA

Fursa mbalimbali za kazi engineering & construction bofya ==> HAPA

Kupata specifications & manual bofya ==> HAPA

Kupata schedules of material, BOQ na excelsheets bofya ==> HAPA

Kupata SEAP reports bofya ==> HAPA

Kama una swali lolote tuwasiliane email: tony.mbugi@must.ac.tz
Previous Post Next Post

Contact Form