📘 Program Maisha Baada ya Chuo Kama Civil Engineer/Technician
Program Hii Ni Maalum Kwa Wahitimu Watarajiwa Civil Engineers/Technicians TU!
Kupitia Program Hii Utaenda Kupata Majibu ya Maswali yote yanayokutatiza na Kukunyima RAHA kama Mhitimu Mtarajiwa Kada ya Civil Engineering Ngazi ya (Diploma au Bachelor) Kila Unapowaza Maisha Baada ya Kumaliza Chuo Kama:
- Nitaanzia wapi baada ya kumaliza chuo, kabla sijaajiriwa na sina mtaji?
- Nitaanzia wapi kutengeneza pesa baada ya kumaliza chuo?
- Jinsi ya kutumia elimu yako ya kitaalamu ya "Civil Engineering" kujikwamua kiuchumi.
- Msingi wa kujiajiri moja kwa moja ikiwa ajira za makampuni binafsi na serikali zitakuwa changamoto.
- Nitapata vipi "connections" zitakazonisaidia kupata kazi?
- Jinsi ya kujenga uzoefu utakao kusaidia kupata kazi katika makampuni makubwa.
- Vitu gani vitakavyomfanya mhitimu wa Civil Engineering aweze kuendesha mradi mpaka mwisho kwa ufanisi?
- Itachukua muda gani kujiajiri au kupata ajira kama Civil Engineer/Technician?
- Je, nianze kufanya kazi inayohusiana na taaluma yangu ya Civil Engineering au kazi yeyote itakayopatikana kwa wakati huo?
- Nitaanzaje au nitaanzia wapi kuishi na kufanya kazi katika taaluma yangu ya Civil Engineering?
- Baada ya kumaliza chuo, nitawezaje kupata fursa za kuendeleza taaluma yangu kabla sijapata ajira?
- Tofauti zilizopo kati ya kufanya kazi kwa mkandarasi, Kujiajiri na kuajiriwa serikalini kama “Civil Engineer/Technician”.
- Ni changamoto gani zipo kwenye soko la ajira kwa sasa?
Je wewe ni civil technician na unajiskia kuchanganyikiwa endapo upo site
na haujui majukumu yako ni yapi kama mtaalamu site.? 😕😕
Asilimia karibia 70% ya wahitimu ngazi ya diploma au bachelor kada ya
civil engineering
wanapomaliza masomo na kupata fursa ya kufanya
kazi sehemu mbalimbali huwa hawajui wala kufahamu majukumu yao hiyo ni
kutokana na sababu ya kutopewa elimu ya awali ya msingi mtu anayotakiwa
afahamu je baada ya kumaliza elimu yake atakaa position gani?.🔰🔰
Usiwe na shaka juu ya ilo hauko pekee yako mimi pia ni mmoja wapo wa watu
ambao nilishawahi kukutana na hiyo hali 😎😄mwaka 2018, baada ya kumaliza
masomo yangu ngazi ya diploma(civil engineering).
👉Kama wewe ni miongoni mwa wahanga wa ilo hapa ulipofika ni mahali
sahihi kabisa na hii makala iko kwa ajili yako..👍
Kabla hatujaendelea na makala yetu naomba uchukue muda wako kidogo
kusapoti channel yangu ya YouTube kwa kubofya ==> HAPA hii inanipa faraja ya kuendelea kukuandalia makala nzuri na za
kujifunza kama hii..🙏
Tunaendelea...
JUKUMU NAMBA 1 : Kusaidia katika kazi za kuandaa michoro ya kazi za site (Help to prepare working drawings)
Kitu cha kwanza unachotakiwa kufahamu hamna kazi yoyote ya ujenzi
inayofanyika bila kuwa na michoro, ndio maana kuna usemi unaosema
"lugha ya wahandisi ni michoro".
Kwaio lazima uliweke ilo katika akili yako wewe ni miongoni mwa watu
unaotakiwa kutoa ushirikiano katika kuandaa michoro ya kazi za site iwe
ni kuandaa plan, section n.k
Hii haipo sana kwa wakandarasi (Contractor)
lakini kama uko upande wa mshauri (Consultancy) hii ni sehemu kabisa ya maisha yako yote.😁
JUKUMU NAMBA 2 : Kuchambua na kutafsiri michoro ya site kwa ajili ya utendaji (Interpret the drawings prepared by architects and engineers)
Kama msimamizi wa site miongoni mwa miongozo inayotakiwa kukusaidia
katika utendaji wa kazi ni michoro hiyo ndo itakuonyesha na kukupa picha
je kazi ikimalizika inatakiwa kuonekana vipi.
Sasa ili uweze kufikia ilo na kufanikiwa lazima uwe unajua kusoma na
kuchambua michoro ili kutoa taarifa sahihi wa watendaji wengine ambao
unawasimamia (skilled & unskilled labours).
Zingatia ilo lazima ujue kusoma mchoro..😃😎 bila hivyo utaibiwa mchana
kweupe..🏃🏃!!
JUKUMU NAMBA 3 : Kujua na kufahamu njia mbalimbali za utenda kazi site (Understand construction techniques and methods)
Huwezi kusimamia ujenzi wa kitu ambacho hata wewe mwenyewe hujui
kinajengwa vipi?😡😡 Kwaio wewe kama mtaalamu na msimamizi wa site lazima
uwe unafahamu njia mbalimbali za ujenzi na namna ya kuitenda kazi.
Mfano kama wewe ni msimamiza wa mradi wa barabara atleast unatakiwa ujue
ujenzi wa barabara unafanyikaje, hatua gani ambazo zinafatwa katika huo
ujenzi mpaka kukamilika, kama unasimamia kazi ya jengo la ghorofa, tenki
la maji vivyo hivyo.
JUKUMU NAMBA 4 : Kufatilia na kusimamia ubora wa kazi kwa viwango vinavyotakiwa (Check and ensure work is done under high quality and specified standards)
Kujua namna na njia mbalimbali za utendaji haitoshi unatakiwa pia
kufatilia na kusimamia ubora wa kazi kwa viwango vilivyoainishwa
kwenye mkataba (specifications).
Kwaio ni jukumu lako kutest ubora wa material mbalimbali ya site kabla ya
matumizi mfano kokoto, matofari, mchanga, kifusi n.k
Na baada ya kazi kufanyika ni jukumu lako kucheck ubora wa kazi kwa
kutest kulingana na viwango vilivyoweka kwenye mkataba.
Kupata specification zitakazo kusaidia kusimamia ubora wa kazi bofya
==>
HAPA
Kupata excelesheet zitakazo kusaidia kutest material bofya ==>
HAPA
JUKUMU NAMBA 5 : Kuandaa schedule of Material kwa ajili ya urahisi wa kupata material kwa wakati bila kuchelewesha kazi (Prepare schedule of materials to easy material ordering and supplying process)
Mkandarasi yoyote anavyokuweka site anataka uwe unajua kuaanda documents
mbalimbali kama Certificate za malipo, Request for Inspection,
B.O.Q
na Schedule of Materials.
Mfano wa sehemu ndogo ya schedule of material;
Hii itasaidia katika kuagiza material zinazohitaji katika utendaji ndani
ya muda na kwa urahisi bila changamoto zozote.
Kuona mfano wa schedule of material iliyokamilika bofya ==> HAPA tafuta kipengele cha construction utapata excelsheet itakayokusaidia kuandaa schedule of material ya
ujenzi wa jengo.
JUKUMU NAMBA 6 : Kupima na kuthaminisha kazi iliyofanya kabla ya kuwalipa mafundi na vibarua (Measuring and valuing work before payment to laborer)
Lazima uwe unajua kupima na kutathmini kazi iliyofanya na mafundi au
vibarua site kabla ya malipo unless otherwise utagombana na boss wako na
kuonekana mtu usiyejielewa.
Na kitu kitachokusaidia hapa ni kujua kusoma mchoro.!! Na vipimo
mbalimbali vya kazi mfano kazi ya kuchimba msingi inapimwa wa urefu, upana
na kina kwaio unachofanya utarudi utaangalia mchoro unatoa vipimo gani?,
Basi wewe utapima kulingana na vipimo vya mchoro.
Labda kazi ya zege inapimwa kwa ujazo (cubic meter) maake tunapima urefu
upana na kina cha structure then tuna vizidisha.
Hivyo ndio inavyotakiwa kuwa.!!
JUKUMU NAMBA 7 : Kuzingatia kanuni na taratibu za usalama kazini (Apply, follow and encourage health and safety rules during site work)
Unatakiwa ufahamu taratibu za usalama eneo la kazi kwa kuwaimiza kutumia
PPE
(Personal Protective Equipments) kama Reflectors, Elements, Safety boot
n.k
Angalia mfano wa mtu aliyevaa vifaa kinga bofya hapa ==>
HAPA
Asilimia takribani 15% za ajali zinazotokea duniani zinatokana na ujenzi
kwaio lazima ulifahamu ilo na kulisimamia kwa sababu
OSHA wanapiga
faini usipokuwa makini kwaio wewe kama msimamizi wa site ilo ni muhimu
kulijua kama miongoni mwa majukumu yako.
Kwaio unatakiwa kumkumbusha msimamizi wako mkuu kuleta vifaa kinga kwa
ajili ya usalama wa watu site.
Simamia profesional yako inavyotakiwa💪💪usionekane mbabaishaji,
kuepuka lawama ambazo ungezipata kama usipolisema ilo kwa msimamizi wako
mkuu (Site engineer).
JUKUMU NAMBA 8 : Kujua namna ya kutumia vifaa mbalimbali vya kazi site na usalama wake (Know how to operate different equipment's safely)
Lazima uwe unafahamu kutumia vifaa mbalimbali wa site kama Level Machine,
Total Station, Theodolite ili hata inapotokea kuna changamoto ya utendaji
uwe msaadawa kwanza kutatua kwa unao waongoza.
Lakini pia lazima usimamie usalama wa hivyo vifaa katika matumizi kwa
sababu sio kila anayepewa kukishika ana utaalamu juu ya matumizi au
usalama wake.
JUKUMU NAMBA 9 : Kusimamia na kuwaongoza watendaji wote wa kazi site vibarua na mafundi ( Organize other building workers)
Lazima ujitambue na kufahamu kuwa wewe ni kiongozi wa vibarua na mafundi
site unaowasimamia kwaio lazima kila siku uwe unawapa na kuwapangia
muelekeo wa kazi siku inayofata ili kila mmoja ajijue akiamkaa anatakiwa
akae wapi na afanye kitu gani.
JUKUMU NAMBA 10 : Kujua na kufatilisha taratibu zote za site kutoka kwa mamlaka husika ( Understand and follow building regulations)
Usifanye ujenzi bila kufata taratibu kwa mamlaka husika, mfano umepewa
kusimamia kazi ya ujenzi wa nyumba usianze ujenzi bila kupata kibali cha
ujenzi kwa mamlaka husika.
==> Hitimisho hayo ndio majukumu na kazi 10 za civil technician site,
natumaini makala hii imekufungua katika utendaji wako na utafanya kazi kwa
ufanisi zaidi ya ilivyokuwa mwanzo.
Kama umenufaika na makala hii sapoti channel yangu ya YouTube kwa
kubofya
==> HAPA
Share makala hii ili na watu wengine wajifunze, kama unaswali lolote basi
liweke kwenye comment hapo chini nitalijibu.
Kwa swali na ushauri zaidi bofya ==>
HAPA
Makala nyingine zaidi;