Kozi zinazotolewa katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) ngazi ya Diploma na vigezo vinavyohitajika.

Kozi zinazotolewa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) 2024/2025

Je, wewe ni mwanafunzi uliyehitimu level ya Form 4 au Form 6 na unatafuta nafasi ya masomo ngazi ya Diploma katika kada za Engineering, Science, Teknolojia au Biashara? 

Au labda wewe ni sehemu ya jamii ya wasomi inayotafuta kupata msukumo kwenye nyanja zinazoendana sera ya nchi inayosema Tanzania ya viwanda yaani nyanja za engineering, science, teknolojia au biashara? 

Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) kinatoa programu mbalimbali kuanzia ngazi ya Certificate, Diploma, Bachelor na Post graduate (Master's & PhD).

Katika makala hii, nimeainisha kozi zote ngazi ya diploma zinazotolewa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) na vigezo vinavyohitajika ili kupata admission  muhula wa masomo 2024/2025.

Je, Unajua.? 💭

Chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) ni chuo kikuu cha sayansi na teknolojia cha serikali Tanzania.

Logo Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST)

[Image Credit: Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) - (source: https://www.must.ac.tz)]

Chuo kina kampasi mbili;

  • Kampasi Kuu (Mbeya mjini)
  • Kampasi ya Rukwa.

Chuo kikuu cha sayansi na teknolojia Mbeya (MUST) kinatoa masomo kuanzia ngazi ya Certificate, Diploma, Bachelor na Post graduate (Master's & PhD).

Chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) kimebase haswa katika kutoa kozi kwenye kada za (Engineering, Science, Teknolojia na Biashara).

Kwa ngazi ya Diploma Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia (MUST) kina toa jumla ya kozi 22 kwa kada zote (Engineering, Science, Teknolojia na Biashara).

Kozi zinazotolewa kwa ngazi ya Diploma katika Chuo Kikuu cha Sayansi Mbeya  (MUST).

  1. Diploma in Business Administration
  2. Diploma in Business Computing
  3. Diploma of Business Administration in Accounting and Finance
  4. Diploma of Business Administration in Marketing and Entrepreneurship
  5. Diploma in Agribusiness with Technology
  6. Diploma in Biotechnology
  7. Diploma in Biomedical Equipment Engineering
  8. Diploma in Information and Communication Technology
  9. Diploma in Laboratory Science and Technology
  10. Diploma in Food Science and Technology
  11. Diploma in Computer Science
  12. Diploma in Architecture
  13. Diploma in Automotive and Auto-electrical Engineering
  14. Diploma in Civil Engineering
  15. Diploma in Computer Engineering
  16. Diploma in Electrical and Electronic Engineering
  17. Diploma in Electronics and Telecommunication Engineering
  18. Diploma in Highway Engineering
  19. Diploma in Mechanical Engineering
  20. Diploma in Mechanical Engineering with Industrial Safety and Occupational Health
  21. Diploma in Mechatronic Engineering
  22. Diploma in Mining Engineering

Vigezo vinavyohitajika ili kupata nafasi ya masomo kwa kozi mbalimbali ngazi ya Diploma katika Chuo Kikuu cha Sayansi Mbeya  (MUST).

Kwa kozi zote za engineering yaani ;-
  • Diploma in Automotive and Auto-electrical Engineering
  • Diploma in Civil Engineering
  • Diploma in Computer Engineering
  • Diploma in Electrical and Electronic Engineering
  • Diploma in Electronics and Telecommunication Engineering
  • Diploma in Highway Engineering
  • Diploma in Mechanical Engineering
  • Diploma in Mechanical Engineering with Industrial Safety and Occupational Health
  • Diploma in Mechatronic Engineering
  • Diploma in Mining Engineering
  • Diploma in Biomedical Equipment Engineering
Kutumia cheti cha form 4, unatakiwa upate ufaula wa pass (alama D) kwenye masomo yako manne kati ya hayo Physcics/Engineering science, Mathematics, Chemistry lazima mawili ya hayo matatu tajwa hapo lazima yawepo.


Kwa kozi zote za Science na Teknolojia yaani ;- 

  • Diploma in Agribusiness with Technology
  • Diploma in Biotechnology
  • Diploma in Information and Communication Technology
  • Diploma in Laboratory Science and Technology
  • Diploma in Food Science and Technology
  • Diploma in Computer Science
  • Diploma in Architecture
Kutumia cheti cha form 4, unatakiwa upate ufaula wa pass (alama D) kwenye masomo yako manne sana sana kwenye masomo ya science yaani Physcics/Engineering science, Mathematics, Geography, Biology, Chemistry lazima mawili kati ya hayo masomo tajwa uwe nayo ongeza na English.


Kwa kozi zote za Biashara yaani ;- 

  • Diploma in Business Administration
  • Diploma in Business Computing
  • Diploma of Business Administration in Accounting and Finance
  • Diploma of Business Administration in Marketing and Entrepreneurship
Kutumia cheti cha form 4, unatakiwa upate ufaula wa pass (alama D) tu kwenye masomo yasiyokuwa ya dini ndani ya hayo manne Mathematics na English ni lazima.


Kufahamu kuhusu ada katika kozi mbalimbali ngazi ya diploma katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) bofya ==> HAPA.

Jinsi ya kufanya maombi Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) bofya ==> HAPA.

Kufahamu zaidi kuhusiana na Fee structure Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) bofya ==> HAPA.

Hitimisho hizo ndizo kozi zinazotolewa katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) ngazi ya diploma na vigezo vinavyohitajika ili upate admission..💥

Sharing is Caring..✌✌

Share kuwafikia watu wengi zaidi na kama unaswali basi unaweza kuuliza kwenye comment section..!!

Unaweza pitia makala hizi nyingine kujifunza zaidi;

Previous Post Next Post

Contact Form