Essential technical skills kwa kila site engineer na technician ili kusimamia mradi wowote bila changamoto.

Nakumbuka kipindi fulani wakati nasimamia mradi wa barabara (Upgrading of Hotelitatu-Mkazambo Road Kilwa District to Gravel Standard) kama site engineer, nilipelekwa borrowpit nikaonyeshwa material mahali pa kuchukua kifusi na layman mmoja hivi nikawa sijui nimwambie operator aanze kuchukua kifusi wapi na wapi aache.?😠

Yule layman akawa kama ndio msemaje mkuu sasa ana muongoza operator mimi nikiwa nashindwa kujua kama kifusi kinafaa au laah nikawa najiuliza mimi kama site engineer kazi yangu ni nini endapo layman ndio mtoa maamuzi, yeye alichokuwa anasema tu kwamba kinatumika ichi ichi kifusi miaka yote.. 

Kuna wakati hadi nikawa naona mbona kama operator anakataa kifusi ambacho ni vumbi kabisa niliduawa mno ila layman yule akawa anasimama kwamba tunatumia hicho hicho, hiyo yote ni kwa sababu nilikuwa nakosa technical skills za site (upande wa materials) yaani kama nikiwa site naweza kujua kwamba haya material yanafaa kwa ajili ya gravel wearing layer au laah.!!

Kwenye makala hii utajifunza essential technical skills ambazo ni muhimu mno kwako kama site engineer na technician ili kusimamia mradi wowote bila changamoto.. 

Kabla hujaendelea kusoma makala hii zaidi naomba usapoti channel yangu ya YouTube ==> HAPA hii inanitia moyo kuendelea kuandaa makala zenye kukupa mwanga kama hizi...🙏👍

Hizi ndizo essential technical skills za site ambazo kila site engineer na technician ili kusimamia mradi wowote bila changamoto. 

1. Kusoma na kutumia standard codes and specifications wakati wa usimamizi.

Hamna mradi wa ujenzi unaofanyika bila kufata specification na standard code (miongozo ya kazi), kila nchi ina miongozo yake kwenye ujenzi (construction) kwaio hata hapa nchini kwetu tuna miongozo inayotusaidia sisi katika kusimamia na kufanya kazi mbalimbali

TARURA wana muongozo wao unaowasaidi katika kusimamia na kutenda kazi, TANROAD vivyo hivyo, National Irrigation Commision (NIC) waona muongozo kwa ajili ya utendaji wa kazi zao, Halmashauri n.k 

Standard code tunazotumia kwa Tanzania hapa ni British Standard na AASHTO. 
💥💥Kupata specification hizi hapa chini 👇👇 bofya ==> HAPA...
1. Pavement and Material Design Manual 1999
2. Road Geometric Design Manual 2012 
3. Tanzania Field Testing Manual 2003 
4. Laboratory Testing Manual 2000 
5. Standard Specification for Road Works 2000 
6. Low Volume Road Manual 2016

2. Materials and material testing.

Ufahamu na ujuzi wa site kuhusiana na material (kokoto, mchanga, mawe, matofari) kuna miradi unatasimamia ambayo haihitaji test za material za mahabara ila wewe kama site engineer au technician lazima ujue je kama hayo material yatafaa kwa ujenzi au laah,

Na hichi ndicho kilichonikuta mimi nilikuwa sifahamu kifusi gani kinafaa kwa matumizi site kwa kukiangalia tu. 

3. Estimation and Costing.

Lazima uwe unajua kufanya makadirio ya kazi (upande wa material na kazi) na gharama, kuna muda utatakiwa ku order material kutoka mbali na kwa gharama ya jua kwaio kama ukiwa una hesabu mbovu itakula kwako.

Kuna muda utasimamia kazi inayotumia mitambo ya kukodi kwaio usipokuwa na makidirio sahihi utajipiga pini..💪 

Kwaio huu ni essential skills mno mno wewe kama site supervisor...✌✌ 

4. Quality control.

Unaposimamia site kuna kazi mbalimbali utazisimamia ikiwa zege, formwork, stone masonry, stone pitching n.k na zote lazima zifanyike katika ubora kwaio kusimamia kiwango cha kazi ni skills muhimu mno, kwa sababu usipokuwa makini utajikuta unaingiza hasara kwa kurudi kazi au kupata kashfa ya kusimamia mradi usiokuwa na viwango. 

5. Kutumia vifaa mbalimbali vya survey.

Vifaa kama levelling machine, Total station, Tape measure unatakiwa ujue namna ya kutumia kwa sababu utakuwa site utatakiwa kupima, kuset level ili kazi iendelee.. 

6. Drawing and design.

Kazi karibia zote a ujenzi (miradi) inafanyika kwa kutumia michoro (drawings) kwaio skills za kuchora na kudesign ni muhimu mno kwako.
Baada ya kazi kuishi utahitajika kuandaa michoro inaitwa A built drawing.
Kwaio skills za drawing and design ni muhimu kwako the big boss..😉😉 
 

7. On field management.

Site utasimamia watu wa ngazi tofauti tofauti mafundi, vibarua (unskilled labour), ma operator,supplier n.k kwaio hao wote lazima ujue namna ya ku deal nao na kuishi nao ili kuhakikisha kazi inaenda vizuri bila changamoto yoyote.
Lazima ujue kutoa tips..motisha ili kazi yako isiwe ngumu..!!😁😀
Mhandisi nakupa mbinu zingatia haya..!!

Hizi ndio essential technical skills kwa kila site engineer na technician ili kusimamia mradi wowote bila changamoto, naamini umejifunza kitu..

Kama umejifunza kitu share na marafiki zaidi ili wajifunze.!

Kujifunza zaidi pitia makala hizi zaidi:-

Previous Post Next Post

Contact Form