Fahamu mambo 3 muhimu ya kuzingatia ili kufanikiwa kwenye interview za engineering & construction -TAMISEMI

Je, wewe ni miongoni mwa watu walioudhuria interview nyingi za TAMISEMI upande wa engineering & construction bila mafanikio 😫😫.? 

Au ni mara yako ya kwanza kuchagulia katika interview TAMISEMI upande wa engineering & construction na hauelewi uanzie wapi 😕😕.?

Fahamu mambo 3 muhimu ya kuzingatia ili kufanikiwa kwenye interview za engineering & construction -TAMISEMI
Kama ni hivyo basi hii makala ipo kwa ajili yako, kabla hatujaendelea naomba chukua muda wako kidogo sapoti channel yangu ya YouTube bofya ==> HAPA 🙏

Pia unaweza kupitia makala hizi kujifunza zaidi;

Katika interview zaidi ya tano za TAMISEMI upande wa engineering & construction nilizokuwa shortlisted na kufanikiwa kuudhuria zaidi ya 60% nilifanikiwa kufika mpaka oral interview.


Unajaribu kutafakari nilizingatia hasa mambo gani.? 💭 

Haya ndio mambo makuu matatu nilizozingatia yaliyoniwezesha kupata mafanikio hayo.

Jambo la kwanza: Elewa majukumu (responsibilities) zote za kazi uliyoiombaa na taasisi uliyoomba majukumu yake kiutendaji.

Ile ujiandae vizuri na interview yoyote ya TAMISEMI upande wa engineering & construction, jambo la kwanza kabisa unalotakiwa kulijua kwa undani ni kujua na kufahamu majukumu ya kazi uliyoomba na sekta uliyoomba inahusika na kazi gani hasa kiutendaji.

Mfano: 
Kazi uliyoomba - Technician (Civil) - II
  • To inspect and reports on roads and bridge maintenance works
  • To supervise road and bridge maintenance works
  • To measure and certifies works for payment
  • To undertake road inventory and condition survey
  • To undertake road traffic count
  • To carry out in situ testing
  • To undertake laboratory tests and to monitor tests results and trends
  • To prepare invoices for materials testing
  • To undertake laboratory apparatus and equipment calibration
  • To prepare site report and
  • To perform such other related duties as may be assigned by the Supervisor.
Taasisi - TANROADS
Majukumu makuu ya taasisi hiyo ni 
  • Road and hydraulic structures construction
  • Road and hydraulic structures maintenance
  • Weighbridges Operation Services
  • Advise/work together with other Road authorities
Kupitia mfano huo jua hapo unapata picha kwamba interview yako ita base hasa upande gani.?😉😉

Jibu => Ni upande wa barabara na miundo mbinu yake.


Jambo la pili : Jua modules zote ulizosoma chuoni zinazohusiana au kushabiiana na jibu ulilolipata hapo juu kwenye jambo la kwanza.

Baada ya kufahamu na kujua majukumu yako na majukumu ya kiutendaji makuu ya taasisi yako.

Kinachofata ni kureview masomo yote uliyoyasoma chuonireferences na manual zote  zinazoshabiiana na jibu ulilolipata kwenye kwenye jambo la kwanza juu pale.

Jibu tuliolipata juu pale interview yetu ita base haswa upande wa barabara na miundo mbinu yake kwaio sehemu kubwa unazotakiwa kupitia na kufanya review moja ni module zote ulizosoma chuoni zinazohusiana na ilo ambazo ni:

  • Road construction and maintenance
  • Pavement design and construction
  • Road geometry design
  • Bridge design & construction
  • Design of hydraulic structures
  • Highway materials
  • Surveying
Mbili manuals zinazotumika hasa katika utendaji wa kazi za barabara ni:
  • Pavement and Material Design Manual 1999
  • Road Geometric Design Manual 2012
  • Tanzania Field Testing Manual 2003
  • Laboratory Testing Manual 2000
  • Standard Specification for Road Works 2000
  • Low Volume Road Manual 2016
Baada ya hapo ni kufanya REVISION... REVISION... REVISION... INTENSIVELY, TIMELY, & PURPOSEFULLY.
!! ... Usizime moto 🔥🔥 ili kupata matokeo ..😊😊

Jambo la tatu : Kama ukifanikiwa kufika Oral interview.

Kama umefanya jambo la kwanza na la pili kwa usahihi zaidi jambo la tatu ni rahisi tu kama kusukuma mlevi 😃😃 kwa sababu asilimia 75% ya maswali utakuwa na uwezo wa kuyajibu.

Unatakiwa tu kuzingatia muda eneo la usahili.

Ukiwa ndani ya chumba cha usahili relax ukiulizwa maswali jibu kwa utulivu, taratibu usiwe na haraka epuka kuongea haraka haraka jiamini.

La mwisho sehemu iliyobaki MUACHIE MUNGU...🙏🙏 wewe kama mwanadamu hivo jua hapo ndio vitu unavyoweza kufanya vyote ndani ya uwezo wako.

Hitimisho hayo ndio mambo 3 muhimu ya kuzingatia ili kufanikiwa kwenye interview za engineering & construction -TAMISEMI


Kama umenufaika na makala hii comment & share ili iwasaidie na wengine.

Kama umenufaika na makala hii naomba muda wako mchache kusapoti channel yangu ya youtube bofya ==> HAPA

Kuona fursa mbalimbali za kazi engineering & construction bofya => HAPA

Kupata reference books & manual bofya => HAPA

Previous Post Next Post

Contact Form