Mambo makuu matatu (3) yanayoku guarantee kupata kazi kwa mkandarasi asilimia 100%.

Nyakati zimebadilika mno..🕖🕖, tuko kwenye nyakati ambazo wanaomaliza ni wengi kuliko soko la ajira, wahitaji ni wengi kuliko uhitaji wenyewe..👷👷

Picha mambo makuu matatu (3) yanayoku guarantee kupata kazi kwa mkandarasi yoyote kwa asilimia 100%


Kiasi unapomaliza masomo kama civil engineer au technician, usipokuwa na connection ya uhakika basi ku survive kwenye industry huwa inakuwa ni changamoto mno..😕

Unatafuta kazi kwa wakandarasi kila kona bila mafanikio au kwa mafanikio madogo, nikisema mafanikio madogo namaanisha utapata kazi lakini watakulipa kidogo, au hawatakulipa kabisa utakuwa kama unajitolea tu..😡😢

Ili kuendana na uhalisia ulivyo hauna budi kubadilika na kuujua ukweli utakao kusaidia kwa kiasi kikubwa na kukupa mafanikio yale ambayo ni matamanio yako...

Je uko tayari kuujua huo ukweli.??👀🙈

Kabla hatujaendelea na makala yetu naomba uchukue muda wako kidogo kusapoti channel yangu ya YouTube kwa kubofya ==> HAPA hii inanipa faraja ya kuendelea kukuandalia makala nzuri na za kujifunza kama hii..🙏

Tunaendelea...

Kabla ya kuwa director wa kampuni ya ujenzi Class V (Civil & Building) - AFRIKWANZA ENGINEERING & CONSTRUCTION LIMITED..


nilipata nafasi ya kufanya kazi na kujifunza haya ninayo kuandika hapa kwa wakandarasi zaidi ya watatu kwa vipindi tofauti ambao ni:

  •  Videfca Construction & Technical Services Ltd 
  •  Maclesence Investment Company  Limited 
  •  Mtwivila Traders & Construction Company Ltd  
  •  Hano Construction Company Limited n.k

Kiukweli saizi makampuni ya wakandarasi yamekuwa ni mengi mno kwa idadi ni zaidi ya 11,952 kutoka na takwimu za Contractors Registration Board (CRB) lakini wanaoweza kukuajiri wewe na kukulipa ni wachache mno ila kitu unachoenda kujifunza hapa kitakupa nafasi ya uhakika wewe kupata hela na kitakupa uwezo wa kufanya kazi na mkandarasi zaidi ya moja popote ulipo.

Haya mambo matatu unayoenda kujifunza hapa huwezi kujifunza darasani, ila ni mambo muhimu mno ambayo ukiwahi kuyajua yanakupa utofauti mkubwa mno na wenzako uliyomaliza nao na yatakuhakikishia kazi kwa mkandarasi yoyote ukiachilia mbali competition ya kukosekana kazi iliyopo mtaani.

Jambo la kwanza: Juu namna ya kumsaidia mkandarasi kupata mradi.

Kama nilivyokuambia hapo awali kuna makampuni mengi mno mno ya wakandarasi lakini wanaopata miradi ni wachache, wewe kama ukiwa na uwezo wa kumsaidia mkandarasi kupata kazi huyo mkandarasi hawezi kukuacha hata siku moja lazima atataka mfanye nae kazi kwa namna yoyote ile, wakandarasi wanatafuta sana watu wa namna hii.

Kuna watu wengi sana wanaoingia kwenye biashara hii ya ukandarasi ambao sio civil engineers wala technicians, civil engineering sio professional yao, mfano mkandarasi nilifanya nae kazi namba mbili kwenye list nilioiorodhesha juu pale director wake alikuwa daktari ila kilicho mvutia kuingia kwenye biashara ya ukandarasi ni kwa sababu tu ana mtaji.

Hivyo ndivyo uhalisia ulivyo, wapo wakandarasi wengi mno wa aina hiyo unachotakiwa kujua wewe ni namna tu ya kumsaidia huyu mkandarasi kupata mradi ukiweza ilo linakuhakikishia kazi nyakati zote kwa sababu wapo wakandarasi wataotaka wakulipe wewe kuwasaidia kuomba na kutafuta miradi.

Najua unaweza ukuwa unajiuliza mimi kama civil engineer au technician namsaidia vipi mkandarasi mwenye hela/mtaji wake kupata miradi.?

Unatakiwa ujue mambo yafuatayo ili uweze kumsaidia mkandarasi  kupata miradi, namna ya kuandaa tender documents fully na vizuri, jua kujaza BOQ vizuri na jinsi ya kutumia mfumo wa kuomba tender (miradi) ==> NEST vizuri ili kupata mradi.

Ukiweza ilo jambo vizuri una uhakika wa kuishi hata kama huja ajiriwa na mkandarasi, kwa sababu wakandarasi watakutafuta tu uwaombe miradi na watakulipa kwa kazi iyo..💰💰

💥💥Kama unahitaji kujifunza ujuzi huu utakaokuhakikishia uhakika wa kupata kazi kwa mkandarasi yoyote yule asilimia 100%, karibu kozi hii inafundisha kwa siku 10 na kila siku utachangia 25,000 ndani ya siku hizo utajifunza kwa vitendo kuandaa tender documents vizuri, kujaza BOQ vizuri na kuomba mradi kwenye mfumo wa NEST 

Bofya button chini hapo palipoandikwa hapa 👍👍 kama unataka kulipia kwa ajili ya kujifunza na kama una swali..💬

Hapa button

Jambo la pili: Ijue kazi na jua jinsi ya kusimamia mradi mwanzo mwisho.

Ukiweza kumsaidia mkandarasi kupata kazi, lazima akipata atakutafuta wewe ukawe msimamizi wa kazi yake, sasa hauwezi kusimamia kitu usichokijua kwaio lazima uijue kazi ili ujihakikishie kupata kazi kwa mkandarasi yoyote yule.

Kuijua kazi namaanisha kama ni barabara ujue ujenzi wa barabara mpaka mwisho na vitu vyote ambavyo vinahusika mpaka mradi kukamilika uwe una uwezo wa kuusimamia ma operator, mafundi na vibarua, kumeneji material na mambo mengine yote ikijumuisha kufanya vikao na client an conultancy wa mradi.

Kuandaa certificate za malipo, kusimamia test za material mpaka kulipwa baada ya kufanya kazi.

Wakandarasi wote wanapenda wapate mtaalamu aliyekamilika yani akikabidhiwa mradi anaua angle zote..😄💪👍 ukiwa hivyo hamna mkandarasi ambae atakuacha.

Najua utakuwa unajiuliza mimi nimamaliza masomo hivi karibuni sina experience nayajuaje yote hayo kwa muda mfupi hivi bofya makala hii hapa chini kujifunza zaidi;

Jambo la tatu: Jua kufanya makadirio ya gharama za mradi mpaka kuisha.

Jambo la mwisho ili litakusaidia kujua kama mradi ukiufanya unakupa hasara au faida, kwaio ni lazima ulijue hii itakusaidia wewe hata ukiwa unafanya kazi na mkandarasi ujue akulipe wewe shingapi.?

ili linaendana na mambo mawili yaliyotangulia hapo juu, ni jambo la kuongezea kwenye mambo mawili hayo juu.

Kujua kufanya makadirio ya mradi itakusaidia kukimbiza kazi ukiwa msimamizi na kufanya menejimenti ya resources ukiwa site.

Hayo ndio mambo makuu matatu (3) yanayoku guarantee kupata kazi kwa mkandarasi yoyote kwa asilimia 100%.

Kama umejifunza kitu share makala hii ili iwafikie watu wengi...🙏🙏

Pia unaweza kupitia makala hizi kujifunza zaidi;

Previous Post Next Post

Contact Form