Kozi zinazotolewa katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) ngazi ya Bachelor Degree na vigezo vinavyohitajika.

Kozi zinazotolewa katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) ngazi ya Bachelor Degree na vigezo vinavyohitajika mwaka wa masomo 2024/2025.

Je, wewe ni mwanafunzi uliyehitimu ngazi ya Diploma au Form 6 na unatafuta nafasi ya masomo ngazi ya Bachelor Degree katika kada za Engineering, Science, Teknolojia au Biashara? 

Au labda wewe ni sehemu ya jamii ya wasomi inayotafuta kujiendeleza ngazi ya Bachelor Degree kwenye nyanja zinazoendana sera ya nchi inayosema Tanzania ya viwanda yaani nyanja za engineering, science, teknolojia au biashara? 

Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) kinatoa programu mbalimbali kuanzia ngazi ya Certificate, Diploma, Bachelor na Post graduate (Master's & PhD).

Katika makala hii, nimeainisha kozi zote ngazi ya Bachelor Degree zinazotolewa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) na vigezo vinavyohitajika ili kupata admission  muhula wa masomo 2024/2025.

Kabla hujaendelea kusoma makala hii zaidi naomba usapoti channel yangu ya YouTube ==> HAPA hii inanitia moyo kuendelea kuandaa makala zenye kutoa msaada kwa jamii kama hizi...🙏👍

Usichokijua kuhusu Chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST).

Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) ni chuo kikuu cha sayansi na teknolojia cha serikali cha pekee Tanzania.

    Logo Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya

    [Image Credit: Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) - (source: https://www.must.ac.tz)]

    Chuo kina kampasi mbili;

    • Kampasi Kuu (Mbeya mjini)
    • Kampasi ya Rukwa.

    Chuo kikuu cha sayansi na teknolojia Mbeya (MUST) kinatoa masomo kuanzia ngazi ya Certificate, Diploma, Bachelor na Post graduate (Master's & PhD).

    Chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) kimebase haswa katika kutoa kozi kwenye kada za (Engineering, Science, Teknolojia na Biashara).

    Ngazi ya Certificate Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia (MUST) kina toa jumla ya kozi 2 kwa kada zote (Biashara).

    Upande wa Diploma Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia (MUST) kina toa jumla ya kozi 22 kwa kada zote (Engineering, Science, Teknolojia na Biashara).

    Level ya Bachelor Degree Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia (MUST) kina toa jumla ya kozi 23 kwa kada zote (Engineering, Science, Teknolojia na Biashara).

    Na ngazi ya Post graduate (Master's and PhD) Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia (MUST) kina toa jumla ya kozi 10 kwa kada zote (Engineering, Science na Teknolojia ).

    Kozi zinazotolewa kwa ngazi ya Bachelor Degree katika Chuo Kikuu cha Sayansi Mbeya  (MUST).

    1. Bachelor of Business Administration
    2. Bachelor of Civil Engineering
    3. Bachelor of Computer Engineering
    4. Bachelor of Electrical Engineering
    5. Bachelor of Engineering in Telecommunication System
    6. Bachelor of Mechanical Engineering
    7. Bachelor of Science in Information and Communication Technology
    8. Bachelor of Technology in Architecture
    9. Bachelor of Technology in Landscape Architecture
    10. Bachelor of Science with Education
    11. Bachelor of Data Science Engineering
    12. Bachelor of Laboratory Science and Technology
    13. Bachelor of Food Science and Technology
    14. Bachelor of Computer Science
    15. Bachelor of Science in Natural Resources Conservation
    16. Bachelor of Agribusiness Management and Technology
    17. Bachelor of Environmental Science and Technology
    18. Bachelor of Science in Biotechnology
    19. Bachelor of Science in Chemistry
    20. Bachelor of Technical Education in Civil Engineering
    21. Bachelor of Technical Education in Mechanical Engineering
    22. Bachelor of Technical Education in Electrical and Electronics Engineering
    23. Bachelor of Technical Education in Architectural Technology

    Vigezo vinavyohitajika ili kupata nafasi ya masomo kwa kozi mbalimbali ngazi ya Bachelor Degree katika Chuo Kikuu cha Sayansi Mbeya  (MUST).

    Kwa kozi zote za engineering yaani ;-
    • Bachelor of Civil Engineering -> (PCM)
    • Bachelor of Computer Engineering -> (PCM)
    • Bachelor of Electrical Engineering -> (PCM)
    • Bachelor of Engineering in Telecommunication System -> (PCM)
    • Bachelor of Mechanical Engineering -> (PCM)
    • Bachelor of Data Science Engineering -> (PCM)
    Kutumia cheti cha ngazi ya Diploma Unatakiwa Uwe Umepata G.P.A ya 3.0 kulingana na course uliyosomea kwenda ile ile unayotaka kuunga Bachelor, kutokea form 6 unatakiwa upate ufaula wa principal pass mbili (alama D) kwenye masomo ya Physcics na Mathematics.

    Kwa kozi zote za Science na Teknolojia yaani ;- 

    • Bachelor of Science in Information and Communication Technology -> (PCM, CBG, PCB, EGM,PMC, PGE & PGM)
    • Bachelor of Technology in Architecture -> (PCM, EGM,PMC & PGM)
    • Bachelor of Technology in Landscape Architecture -> (PCB, PCM & PGM)
    • Bachelor of Science with Education -> (PCM, CBG, PCB, EGM,PMC & PGM)
    • Bachelor of Laboratory Science and Technology -> (CBG & PCB)
    • Bachelor of Food Science and Technology -> (PCM, CBG & PCB)
    • Bachelor of Computer Science -> (PCM, PMC & PGM)
    • Bachelor of Science in Natural Resources Conservation -> (CBG & PCB)
    • Bachelor of Agribusiness Management and Technology -> (Masomo ya Science, Art & Biashara)
    • Bachelor of Environmental Science and Technology -> (PCM, CBG, PCB, EGM,PMC & PGM)
    • Bachelor of Science in Biotechnology -> (PCM & PCB)
    • Bachelor of Science in Chemistry ->  Chemistry lazima tahasusi (PCM, CBG & PCB)
    Kutumia cheti cha ngazi ya Diploma Unatakiwa Uwe Umepata G.P.A ya 3.0 kulingana na course uliyosomea kwenda ile ile unayotaka kuunga Bachelor, kutokea form 6 unatakiwa upate ufaula wa principal pass mbili (alama D) kwenye tahasusi nilizoorodhoshe mbele hapo.

    Kwa kozi zote za Biashara yaani ;- 

    • Bachelor in Business Administration -> Masomo ya Art, Science, Language na Biashara
    Kutumia cheti cha ngazi ya Diploma Unatakiwa Uwe Umepata G.P.A ya 3.0 kulingana na course uliyosomea kwenda ile ile unayotaka kuunga Bachelor, kutokea form 6 unatakiwa upate ufaula wa principal pass mbili (alama D) kwenye masomo ya Art, Science, Language na Biashara.

    Kwa kozi zote za Technical Education yaani ;- 

    • Bachelor of Technical Education in Civil Engineering -> (PCM, CBG, PCB, EGM,PMC & PGM)
    • Bachelor of Technical Education in Mechanical Engineering -> (PCM, CBG, PCB, EGM,PMC & PGM)
    • Bachelor of Technical Education in Electrical and Electronics Engineering -> (PCM, CBG, PCB, EGM,PMC & PGM)
    • Bachelor of Technical Education in Architectural Technology -> (PCM, CBG, PCB, EGM,PMC & PGM)

    Kutokea form 6 unatakiwa upate ufaula wa principal pass mbili (alama D) kwenye masomo ya science .

    Kufahamu kuhusu ada katika kozi mbalimbali ngazi ya diploma katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) bofya ==> HAPA.

    Jinsi ya kufanya maombi Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) bofya ==> HAPA.

    Kufahamu zaidi kuhusiana na Fee structure Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) bofya ==> HAPA.

    Hitimisho hizo ndizo kozi zinazotolewa katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) ngazi ya Bachelor Degree na vigezo vinavyohitajika ili upate admission..💥

    Sharing is Caring..✌✌

    Share kuwafikia watu wengi zaidi na kama una swali basi unaweza kuuliza kwenye comment section..!!

    Unaweza pitia makala hizi nyingine kujifunza zaidi;

    Previous Post Next Post

    Contact Form