Mambo 3 ya Kufanya Civil Engineer/Technician Baada ya Kutafuta Ajira Serikalini Bila Mafanikio.

Truth be told always...

Soko la ajira ni gumu mno mno, wahitimu na wahitaji wa ajira ni wengi kuliko nafasi za ajira zinazopatikana.!

Kuna wakati unaweza kutafuta ajira kwenye makampuni binafsi au serikarini kwa muda mrefu bila mafanikio.

Picha Mambo 3 ya Kufanya Civil Engineer/Technician Baada ya Kutafuta Ajira Serikalini Bila Mafanikio.
Kuna watu toka wamalize masomo wame attend interview nyingi za Tamisemi (Engineering & Construction) kwa miaka mingi bila mafanikio.

Wamekaa mtaani muda mrefu na kukataa tamaa kabisa, na wengine wamepoteza direction kabisa wakiamini kuwa wamepoteza tu muda wao kwenda chuo.

Ofcourse hali hiyo hata mimi mwenye ili wahi kunikuta miaka miwili nyuma baada ya kuona nafanya kazi kwa wakandarasi bila mafanikio yoyote hamna nacho gain changamoto ni nyingi, ugumu ndio unazidi kwa kila jitihada.

Nilianza kutafuta ajira permanent za serikali, niliattend interview kaza ofcourse kwa mafanikio makubwa kwa sababu karibia interview zote za Tamisemi (Engineering & Construction) nilizo attend nilifanikiwa kufika oral interview stage.

Kujua mbinu nilizotumia zikanipa hayo mafanikio soma makala hii hapa chini..

Ofcourse ukiwa bado hujapata ajira kuna perspective (taswira) fulani unakuwa nayo kichwani, baada ya kusaka ajira wee bila mafanikio kiasi unashindwa kuona fursa upande wapili wa mambo.

Kwenye makala hii utajifunza mambo 3 ya kufanya civil engineer/technician baada ya kutafuta ajira serikalini bila mafanikio.

Mambo unayoenda kujifunza hapa ni mambo nilijifunza by experience baada ya kuwa muajiriwa wa serikali nakupata taswira nyingine mpya ambayo nilikuwa sina hapo awali wakati nasakaa ajira.

Haya ndio mambo matatu 3 ya kufanya wewe kama civil engineer/technician baada ya kutafuta ajira serikalini bila mafanikio.

Jambo la kwanza : Kaongeze elimu yako 📚📚

Najua kuna watu hawatakubaliana na mimi, ila nataka nikuhakikishie mimi nimeajiriwa lakini naona fursa nyingi mno za ajira zipo kama mtu atachukua hatua na kufanya maamuzi ya kwenda kuongeza elimu yake.

Mfano kama una bachelor, nenda kaongeze elimu yako kufikia ngazi ya masters kuna fursa nyingi mno zipo kwa watu walio ngazi ya masters.

Bachelor na diploma siku hizi zimekuwa nyingi kama ndala tu kiasi competition ya watu ni kubwa kwa sababu watu wenye ngazi hizo za elimu diploma na bachelor ya civil engineering ni wengi mno mno..

Ila unapoongeza elimu kwenda juu competition ina pungua na wanaohitajika wenye level hiyo ya elimu wanakuwa wengi ila ambao wapo ni wachache.

Hiki nachozungumza siyo maneno tu ni kitu ambacho nimekifanyia utafiti ndani ya mwaka nikiwa kazini na fursa nazo ziona mbele kwa watu wote walioamua kuongeza elimu zao.

Jambo la pili : Jifunze skills zenye uhitaji na ufundi mbalimbali (crafts kama plumbing, steel fixing etc.)

Ofcourse mfumo wa masomo ulivyo kwa watu wanaofanya masomo ya diploma and bachelor in civil engineering unatengeneza watu wengi ambao hawajui kazi za mikono, wakiwa site hawana wanachoweza kukifanya wenyewe kwa mikono yao zaidi ya kusimamia watu wengine na kufanya kazi za menejimenti zaidi kuliko kazi zinazozalisha na kuleta matokeo ya moja kwa moja kwenye utendaji.

Ukiwa una ujuzi wa ufundi ndani yake jumlisha elimu yako una nafasi kubwa ya kupata kazi nyingine nyingi nje ya kile ullichosomea.

Lakini pia hata ukiwa muajiriwa kumbuka msharaha nikitu fixed hakikui ili kujiongeze thamani zaidi na kuwa na means nyingine ya kuzalisha pesa jifunze skills zenye uhitaji na ufundi utakao kuwezesha wewe kutoa huduma kwa watu one on one na watu watakuwa tayari kukulipa kwa ilo.

Jambo la tatu : Jifunze uwekezaji na biashara mbalimbali.

Usikae kung'ang'ania tu elimu yako na kuikumbatia kama haikupi mafanikio yoyote ni wakati wakuiacha na kujaribu kufanya vitu vingine nje na elimu au sekta yako.

Kuna biashara nyingi tu ambazo watu wanahitaji huduma huko nje, tumia fursa hiyo kuifanya.

Vijijini mbali na miji wako watu wanahitaji bidhaa nyingi za umeme, afya, chakula, nishati n.k anza kutoa huduma ya hivyo vitu kwa mtaji wowote ule wakukopa, kuazima, kufanya vibaruan.k.

Jifunze kuangalia fursa..

Mfano mahali naishi mimi kuna changamoto kubwa ya watu kuzalisha taka lakini wanashindwa jinsi ya kuzimanage yaani zinazagaa tu ovyo mtaani, lakini kuna fursa mtu akaiwa yuko tayari anweza anzisha huduma ya kuzkusanya hizo taka na kuzipeleka mahali husika na watu wakamlipa hela kwa ilo.

Kama unaona biashara na kitu kigumu kwako jifunze uwekezaji anza kuwekeza kwenye sekta ya ufugaji n.k

Kujifunza kuhusu uwekezaji kwako kama civil engineer au technician soma makala hii.

Haya ni mambo matatu niliyojifunza ambayo yanaweza kuwa msaada kwako na muongozo, kama umefurahia makala hii basi naomba sapoti yako kwa ku bofya ==> HAPA hii inanipa faraja mimi ya kukuandalia makala kama hizi zenye kukusaidia..🙏

Soma makala nyingine hizi kujifunza zaidi.. 

    Previous Post Next Post

    Contact Form